6.22.2016

0

WOSIA NA VITU VYA KUZINGATIA WAKATI WA UANDAAJI WA WAKE TANZANIA


Wosia  na Vitu vya Kuzingatia Wakati wa Uandaaji wake Tanzania
Utangulizi
Wosia ni nini?
Wosia ni kauli ama tamko analolitoa mtu wakati wa uhai wake kwa hiari akieleza ni nini kifanyike baada ya kifo chake,pia huonyesha nia yake jinsi gani  mali zake zigawanywe baada ya kufa kwake,katika wosia muusia anaweza pia kutamka ni wapi azikwe baada ya kifo chake.
Aina za Wosia
Kuna aina kuu mbili za wosia nazo ni;
i.wosia wa maandishi
ii.wosia wa mdomo(usio wa mandishi).
Wosia wa maandishi ni wosia ambao huandikwa kw maneno katika karatasi na wosia wa mdomo ni wosia ambao muusia haandiki wosia wake katika ila husema kwa mdomo tu,
Wosia wa Maandishi
Ili wosia wa maandishi ukubalike kisheria lazima uwe na vitu vifuatavyo;
Uandikwe katika karatasi nyeupe na uandikwe kwa kalamu isiyofutika yaani ya wino na si ya risasi.Anayetoa wosia awe na akili timamu na ataje kama ana hakili timamu na pia aonyeshe kama alitoa wosia kwa kwa hiari yake.Ushuhudiwe na mashahidi wanaojua kusoma na kuandika angalau wawili (mmoja wa ukoo na mwingine mtu baki) hii ni pale muusia anapokuwa anajua kusoma na kundika.Na pia kama muusia hajui kusoma na kuandika ushuhudiwe na watu wanne (wawili kwa ukoo na wawili watu baki).Wanaotarajia kurithi au watu wenye maslahi na wosia huo hawatakiwi kushudia. Wosia huo usainiwe na muusia mbele ya mashahidi wake wakiona,akitia saini yake na kama hjui kusoma na kuandika basi atie alama ya kidole gumba chake cha kulia.Mashahidi pia watie saini zao.Mashahidi lazima wawe wammechaguliwa na muusia mwenyewe.

Wosia wa Mdomo
Vitu vya kuzingatia wakati wa kuandaa wosia wa mdomo
Ushuhudiwe na mashahidi wanne (wawili wa ukoo na wawili watu baki)Mashahidi wawe wamechaguliwa na muusia mwenyewe Muusia awe na akili timamuKama mashahidi watakufa kabla ya muusia kufa basi wosia hautkubalika na urithi utagawiwa kadri ya mpango wa urithi usio wa wosia.
Angalizo,wosia unaweza kubatilishwa pale ambapo utatolewa bila kuzingatia mambo ya msingi.
Faida za Wosia
Muusia anapata fursa ya kugawa mali zake kwa watu anaotaka wagawiwe.Wosia unaepusha ugonvi na migogoro baina ya nduguMuusia anapata fursa  ya kuamua ni nani awe msimamizi wa mali zakeMuusia anapata fursa ya kuchaguaa azikwe wapi
Mahali pa kutunza wosia
Wosia unatakiwa utunzwe sehemu salama,sehemu hizo ni kama benki,kwa mwanasheria,mahakamaani au kwa mtu yeyote ambaye muusia anamwamwini.
Hitimisho,watu wanashauriwa kuandaa wosia wakati wa uhai wao,watu waache uchuro hii ni kwasababu wosia una faida sana kwa muusia na wale wanaobaki.
Marejeo,
Chama cha wnasheria Tanzania bara
 





0 comments:

Post a Comment